IDARA YA KILIMO NA UMWAGILIAJI
2.1. UKANDA WA CHINI:
Ukanda huu una mwinuko wa meta 900 – 1,200 kutoka usawa wa bahari, hupata mvua chache kiasi cha mm 500 – 600 kwa mwaka na kiwngo cha joto ni kati ya 20 °c – 30 °c.
Ukanda huu unajumuisha maeneo ya Tarafa za Pawaga, Idodi na Isimani. Mazao yanayoliwa ni pamoja na mahindi, mpunga, vitunguu, nyanya, ndizi, karanga, pamba, mtama, mhogo, maembe, machungwa, korosho, mapapai, ufuta na viazi vitamu.
2.2. UKANDA WA KATI:
Ukanda huu una mwinuko wa meta 1,200 – 1,600 kutoka usawa wa bahari, hupata mvua za wastani na juu ya wastani mm 600 – 1,000 kwa mwaka na kiwango cha joto ni kati ya 15 °c – 20 °c.
Ukanda huu unajumuisha maeneo ya Tarafa za Mlolo, Kalenga, Kiponzelo na Kata za Kising’a na Kihorogota katika Tarafa ya Isimani. Mazao yanayolimwa ni tumbaku, alizeti, kabeji, ngano, soya, mahindi, pamba nyanya, viazi vitamu, viazi mviringo, maharage, ufuta, mboga na matunda. Mazao mengine yanayoweza kustawi ni kahawa, pareto na njegere.
WATUMISHI:
Idara ya Kilimo, Umwagiliaji na Ushirika ina jumla ya watumishi 94 ambapo kati yao watumishi 22 wako Makao Makuu na watumishi 72 wapo ngazi ya Vijiji na Kata.
SHUGHULI ZINAZOFANYIKA IDARANI:
Kupanga na kusimamia mpango wa utoaji wa huduma za ugani (Agriculture Education and Extension Services) katika Wilaya kwa kushirikiana na wadau mbalimbali.
Kutoa mafunzo mbalimbali kwa wakulima juu ya kanuni bora za uzalishaji wa mazao kwa njia ya mashamba ya mfano, mashamba darasa maonesho kama vile maadhimisho ya Nanenane, semina, n.k.
Kusimamia utendaji kazi wa watumishi na kuhakikisha wanapata maslahi yao.
Kusimamia upatikanaji na usambazaji wa zana za kilimo na pembejeo ili kuongeza tija katika uzalishaji wa mazao.
Kusimamia na kutoa elimu ya uzalishaji wa mazao ya chakula, biashara, mboga na matunda ili kuwawezesha wakulima kuwa na uhakika wa chakula na kuongeza kipato katika kaya.
Kuandaa mpango wa matumizi bora ya ardhi katika kilimo na kushauri viwango vya matumizi ya pembejeo muhimu kama mbolea kufuatana na rutuba ya udongo.
Kusimamia upatikanaji wa viuatilifu na kutoa elimu ya udhibiti wa visumbufu vya mazao kama panya, ndege, wadudu na magonjwa katika mazao.
Kutoa elimu ya ushirika na kusimamia vyama vya ushirika vya Mazzo AMCOS, SACCOS na vikundi vilivyosajiliwa rasmi.
Kutoa elimu ya matumizi na uchanganyaji wa vyakula ili kuboresha lishe katika jamii.
Ukusanyaji wa taarifa muhimu za uzalishaji wa mazao, mwenendo wa mvua nakadhalika kwa ajili ya kutoa ushauri kwa wakulima.
Kusimamia ujenzi na matumizi sahihi ya miundombinu ya kilimo hususani maghala na skimu za Umwagiliaji kwa ajili ya kuiwezesha jamii kuongeza uzalishaji na kuboresha hifadhi ya mazao hasa ya nafaka.
MATANGAZO:
5.1. UVUNAJI, UTUNZAJI NA MATUMIZI BORA YA CHAKULA:
Tangazo hililimetolewa tarehe 09/09/2016 kwa wananchi kupitia Maafisa Watendaji wa Kata. Tangazo linasisitiza umuhimu wa wananchi kujiwekea akiba katika kaya ili kuepuka upungufu wa chakula. (Kiambatishi “A).
5.2. MWELEKEO WA MSIMU WA MVUA 2016:
Tangazo limetolewa kwa wananchi tarehe 13/10/2016 kupitia Watendaji wa Kata kusisitiza wananchi walime mazao yanayovumilia ukame kama mtama. viazi vitamu, mihogo, mbaazi na mazao mengine yanayokomaa kwa muda mfupi na kuwakumbusha wananchi kuhifadhi chakula cha kutosha misimu miwili. (Kiambatishi “B”).
Maelekezo hayo yametolewa kutokana na Mamlaka ya Hali ya Hewa Tanzania kutoa taarifa kuwa mvua zinatarajia kuanza wiki ya pili ya mwezi Disemba 2016 na zinatarajia kuwa chini ya wastani hadi wastani katika maeneo mengi ya Nyanda za Juu Kusini.
5.3. TATHMINI YA HALI YA CHAKULA:
Tangazo limetolewa kwa wananchi tarehe 10/02/2017 kupitia Watendaji wa Kata kufahamu hali ya upatikanaji wa chakula katika Vijiji na Kata zote katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa kuanzia Februari, 2017 (Kiambatishi “C”).
Lengo likiwa ni kujua hali halisi ya chakula na kuweka mipango ya baadaye.
MIRADI YA KILIMO INAYOTEKELEZWA KATIKA KIPINDI CHA 2016/2017:
6.1. MIUNDIMBINU YA UMWAGILIAJI:
Ujenzi wa skimu za Umwagiliaji unaendelea katika maeneo ya Mlambalasi, Mafuruto na Mkombilenga. Mradi wa ujenzi wa skimu ya Mafuruto unafadhiliwa na Tanzania/Japan Food Aid Cuonterpart (FACT) kwa gharama ya Tshs. 350,000,000.000
Ujenzi wa Skimu ya Mlambalasi unajengwa kwa fedha kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia mfuko wa “Small Scale Irrigation Development Project (SSIDP)” kwa gharama ya Tshs. 249,208,330.00.
Ujenzi wa Skimu ya Mkombilenga unajengwa kwa fedha kutoka Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia mfuko wa “Small Scale Irrigation Development Project (SSIDP)” kwa gharama ya Tshs. 651,863,506.00.
6.2. MIUNDOMBINU YA HIFADHI YA MAZAO:
Maghala mawili yamejengwa katika msimu 2016/2017 katika Vijiji vya Magozi na Tungamalenga kwa ajili ya kuhifadhi mpunga wa wakulima. Maghala hayo yamejengwa kwa fedha za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kila moja likiwa na uwezo wa kuhifadhi Tani 5,000 za mpunga. Ghala la Magozi limegharimu kiasi cha Tshs. 682,330,000.00 na ghala la Tungamalenga limegharimu kiasi cha Tshs. 776,311,250.00.
Mtaa wa Gangilonga
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0754 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa