Mkuu wa Mkoa wa Iringa, Mhe Ally Hapi ameanza ziara yake ya kukagua miradi ya maendeleo na kusikiliza kero za wananchi katika Tarafa ya Mlolo,Kiponzero na Kalenga ikiwa ni muendelezo wa ziara yake ya Tarafa kwa Tarafa Wilayani Iringa.
Katika ziara hiyo, Mhe Hapi ametembelea na kukagua Ujenzi wa mradi wa maji (WARIDI), ujenzi wa Hostel Sekondari Isimila, Kukagua barabara ya Tanangozi – Makongati, ujenzi wa madarasa matatu (3) na Matundu sita (6) ya Vyoo Shule ya Msingi Makota, Kukagua mradi wa maji Ifunda, Kukagua ukarabati wa shule ya sekondari Ifunda Tech , Kukagua ukarabati wa mabweni nane (8) Ifunda Girls, Kukagua ujenzi wa barabara ya Ifunda - Kiponzero , Kukagua mradi wa maji wa Isupilo - Itengulinyi , Kukagua ujenzi wa madarasa matatu (3) na matundu Sita (6) ya vyoo Shule ya Msingi Msukanzi Kukagua ujenzi wa madarasa matatu (3) na matundu sita (6) ya vyoo Shule ya Msingi Lyalamo, Kukagua huduma za afya Hospitali ya Tosamaganga, Kukagua ujenzi wa mradi wa maji magubike (WARIDI),na kumalizia kwa mkutano wa hadhara pamoja na kusikiza kero za wananchi maarufu (mahakama ya wananchi) ambazo zitajibiwa na wakuu wa Idara wa Halmashauri na Mameneja wa Mashirika mbalimbali.
Mkuu wa Mkoa yupo siku ya tatu ya ziara yake ya siku sita kutembelea Tarafa sita za Wilaya ya Iringa.
Mtaa wa Gangilonga
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0754 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa