Waandishi wa habari wa Mkoa wa Iringa wametakiwa kuwa kiunganishi kati ya Serikali na Wananchi wake kwa kuibua changamoto na matatizo yanayowakabili wananchi na kuyatafutia muendelezo wake baada ya kuyaibua.
Hayo yamesemwa na Katibu Tawala wa Wilaya ya Iringa Ndg Hashimu Komba wakati wa hafla fupi ya kuwashukuru Waandishi wa Habari wa Mkoa wa Iringa walioshiriki katika Ziara ya Mkuu wa Mkoa wa Iringa .
Komba amesema kuwa vyombo vya habari ni Mdau muhimu katika kuifanya Serikali kutimiza majukumu yake kwa kuweza kuonyesha kuna changamoto gani ndani ya jamii kupitia media, hivyo media inapoibua jambo au changamoto ni vyema muendelezo wa lile jambo ukaonekana ili Serikali iweze kulifanyia kazi kwa haraka huku akiwakumbusha waandishi hao kuepukana na ile dhana ya kufanya kazi na Serikali kwa kuviziana.
“Nyinyi ni watu wa muhimu sana,tuendelee kuwaomba ushirikiano katika kufanya kazi na Serikali,muwe huru kutoa maoni na changamoto ambazo mnakutana nazo mnapofanya kazi na Serikali na muwe kiunganishi kati ya Wananchi na Serikali,niwashukuru sana kwa namna mlivoshiriki na kuripoti ziara ya Mkuu wa Mkoa,ushirikiano huu udumu na Mungu awabariki”, alimaliza Ndg Komba.
Mkuu wa Mkoa wa Iringa Mhe. Ally Hapi amemaliza ziara yake katika Halmashauri ya Wilaya ya Iringa ambapo alikagua Miradi ya Maendeleo yenye thamani ya shilingi bilioni 19,017,662,792,na kusikiliza kero za Wananchi katika Tarafa za Pawaga,Kalenga,Idodi,Mlolo,Ismani na Kiponzero.
Mtaa wa Gangilonga
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0754 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa