Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa amewaonya Watanzania wanaosafirisha dawa za kulevya nchini kwa njia mbalimbali ikiwemo kumeza tembe za dawa hizo tumboni kwa madhumuni ya kuzipeleka nje ya nchi, wameaswa kuacha vitendo hivyo mara moja,la sivyo wakikamatwa na kutiwa hatiani cha moto watakiona.
Waziri Mkuu ameyasema hayo mapema jana wakati wa Maadhimisho ya Kitaifa ya Siku ya Kupiga vita dawa za kulevya yaliyofanyika Kitaifa Mkoani Iringa.
Waziri Majaliwa amewaonya Wananchi kutojihusisha kabisa na matumizi wala biashara ya madawa ya kulevya,kwani biashara hiyo ni haramu na haikubaliki duniani na hata dini zote zinaipinga vikali.
Mtaa wa Gangilonga
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0754 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa