• Malalamiko |
    • Wasiliana nasi |
    • MMM |
    • Barua Pepe Za Watumishi |
Iringa District Council
Iringa District Council

Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Ofisi ya Rais,Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Halmashauri ya Wilaya ya Iringa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Historia
    • Dira na Dhima
    • Maadili ya Msingi
    • Mikakati
  • Utawala
    • Muundo wa Halmashauri
    • Idara
      • Utawala na Rasilimali watu
      • Fedha na Biashara
      • Mipango Takwimu na Ufuatiliaji
      • Maendeleo ya Jamii
      • Afya
      • Elimu sekondari
      • Elimu Msingi
      • Ujenzi
      • Ardhi na Maliasili
      • Kilimo umwagiliaji na ushirika
      • Mazingira na Usafishaji
      • Serikali za Mitaa
      • Maji
    • Vitengo
      • TEHAMA NA Uhusiano
      • Sheria
      • Ukaguzi wa ndani
      • Ugavi na Manunuzi
      • Uchaguzi
      • Ufugaji Nyuki
  • Fursa za Uwekezaji
    • Vivutio vya Utalii
    • Kilimo
    • Ufugaji
  • Huduma zetu
    • Afya
    • Elimu
    • Maji
    • Kilimo
    • Ufugaji
    • Uvuvi
  • Madiwani
    • Orodha ya Madiwani
    • Kamati za Kudumu
      • Mipango,Utawala na Uchumi
      • UKIMWI
      • Afya Elimu na Maji
      • UMazingira, uchumi na Ujenzi
      • Maadili
    • Ratiba Ya Vikao mbalimbali
      • Vikao vya Waheshimiwa Madiwani
      • Kuonana na Mwenyekiti wa Halmashauri
  • Miradi
    • Miradi iliyopangwa kutekelezwa
    • Miradi inayoendelea
    • Miradi iliyokamilika
  • Machapisho
    • Sheria Ndogo
    • Mkataba wa Hudumakwa Wateja
    • Mpango Mkakati
    • Ripoti
    • Fomu
    • Miongozo
  • Kituo cha habari
    • Taarifa kwa vyombo vya Habari
    • Video za Shughuli Mbalimbali za kiofisi na za Kitaifa
    • Hotuba za Viongozi Mbalimbali
    • Maktaba ya Picha

Inayoendelea

2. 0 HALI YA UTEKELEZAJI WA MIRADI ILIYOKAGULIWA HALMASHAURI YA WILAYA YA IRINGA MAY 2018

 

                        2.1 SEKTA YA ELIMU MSINGI

NA

JINA LA MRADI

MAHALI ULIPO

HALI HALISI YA UTEKELEZAJI

FEDHA ILIYOTOLEWA

MATUMIZI HALISI

BAKI

MAONI

2.1.1
Ujenzi wa madarasa matatu (3) na matundu 6 ya vyoo katika shule ya msingi Mkungugu.
Kijiji cha Mkungugu
Ujenzi wa madarasa 3 na ofisi 1 upo katika hatua ya umaliziaji (finishing). Kazi zinazoendelea kupiga plasta, kuweka milango, dari, kuweka sakafu na utengezaji wa madawati unaendelea. Utekelezaji umefika asilimia 85.

66,600,000

50,657,500

15,942,500

Timu ya Ukaguzi inashauri kasi ya ujenzi iongezwe ili ujenzi ukamilike haraka kulingana   na muda uliotakiwa. Pia timu inashauri wahakikishe ujenzi unakamilika haraka kulingana na muda uliotakiwa. Aidha fedha ya ujenzi wa vyoo iliyoombwa kubadilisha matumizi ifuatiliwe ili itumike kukarabati madarasa mengine yaliyochakaa.
2.1.2
Ujenzi wa madarasa matatu (3) na matundu 6 ya vyoo katika shule ya msingi Mboliboli
Kijiji cha Mboliboli
Ujenzi wa madarasa 3 kuta zimeshainuliwa na kumiminwa bimu. Kazi zinazoendelea upigaji wa plasta, kumwaga jamvi la chini (zege) na ununuzi wa vifaa vya umaliziaji unaendelea. Ujenzi wa matundu 6 ya vyoo shimo limeshachimbwa, linatakiwa kufanyiwa marekebisho kulingana na BOQ. Utekelezaji umfikia asilimia 45.

66,600,000

22,790,000

43,810,000
Kutokana na mradi huu kasi yake kuonekana ndogo, timu ya ukaguzi inashauri Afisa Elimu Msingi (W) na Mhandsi wa ujenzi (W) wafanye ufuatliaji wa karibu kuhakikisha wanaongeza kasi ili ujenzi ukamilike kwa wakati kama ilivyotakiwa kwani bado wapo nyuma katika utekelezaji. Aidha fundi mkuu alishauriwa kuongeza idadi ya mafundi na vibarua ili waendelee na ujenzi wa matundu ya vyoo kama ilivyotakiwa.
2.1.3
Ujenzi wa madarasa matatu (3) na matundu 6 ya vyoo katika shule ya msingi Lyalamo
Kijiji cha Tosamaganga
Ujenzi wa madarasa 3 yameshapauliwa na kupigwa lipu nje na ndani, sakafu imeshawekwa na dari. Kazi zilizobaki kuweka madirisha, milango na hatua nyingine za umaliziaji.  Ujenzi wa vyoo, kibanda kimeshapauliwa, kazi zinazoendelea kumalizia uchimbaji wa shimo. Utekelezaji umefikia asilimia 89.

66,600,000

48,139,200

18,460,800

Ujenzi wa matundu 6 ya vyoo utaunganishwa kwenye shimo la zamani kutokana na eneo kuwa dogo la ujenzi, hivyo timu ya ukaguzi imemshauri Mhandisi wa Ujenzi (W) na kamati ya ujenzi ya shule kama kutakuwa na kiasi kitakachobaki watengeneze miundombinu kwa ajili ya watoto wenye mahitaji maalumu kuweza kufika mahali choo kilipo. Pia timu ya ukaguzi inashauri kufanyike marekebisho kwenye sakafu zote zilizowekwa kwenye madarasa 3 kwani hakuna slope ya kuwezesha maji yatoke kirahisi na kusababisha maji kutuama.
2.1.4
Ujenzi wa madarasa matatu (3) na matundu 6 ya vyoo katika shule ya msingi Makota
Kijiji cha Makota
Ujenzi wa madarasa 3 kuta zimeshainuliwa na kumiminwa bimu. Ujenzi wa matundu 6 ya vyoo shimo limeshachimbwa. Utekelezaji umefikia asilimia 35

66,600,000

17,861,500

48,738,500

Wakati wa ukaguzi hakukuwa na kazi inayoendelea na pia mafundi hawakuwepo site. Kutokana na utekelezaji kuwa nyuma timu ya ukaguzi wa miradi imeshauri mafundi waongezwe, pia kwa wananchi wamefanya kazi kubwa ya uchimbaji shimo, ukusanyaji mawe na tofali, hivyo kuna uwezekano wa kiasi cha fedha kubakia na kuongeza idadi ya matundu mawili ya choo na kufikia matundu 8.
2.1.5
Ujenzi wa madarasa matatu (3) na matundu 6 ya vyoo katika shule ya msingi Msukanzi
Kijiji cha  Tosamaganga
Ujenzi wa madarasa 3 yameshapauliwa na kupigwa lipu nje na ndani, sakafu imeshawekwa na dari. Kazi zilizobaki kuweka madirisha, milango na hatua nyingine za umaliziaji.  Ujenzi wa vyoo matundu 6, kibanda kimeshapauliwa, kazi zinazoendelea kupiga lipu nje na ndani na hatua nyingine za umaliziaji. Utekelezaji umefikia asilimia 88.

66,600,000

56,497,400

10,102,600
Timu ya ukaguzi inashauri Mtendaji wa kijiji kuhakikisha wananchi wake wanamalizia uchimbaji wa shimo la choo kama ilivyotakiwa.

 
2.2 SEKTA YA ELIMU SEKONDARI




2.2.1
Ukarabati wa Mabweni 8 na matundu 16 ya vyoo katika shule ya sekondari ya Wasichana Ifunda
Kijiji cha Ifunda
Mabweni 8, na Matundu 16 ya vyoo vya Wanafunzi yamekarabatiwa. Utekelezaji umefikia asilimia 100.

106,416,000

106,416,000

0

Zikipatikana fedha nyingine ufanyike ukarabati kwa kupaka baadhi ya kuta rangi ambazo zinaoneka rangi zake kufifia.
2.2.2
Ujenzi wa madarasa 3 na matundu ya vyoo 5 katika shule ya sekondari Kiwele
Kijiji cha Mfyome
Ujenzi wa Madarasa 3 upo katika hatua za mwisho za umaliziaji (finishing) kwa kupaka rangi, kuweka vioo vya madirisha na kutengeneza madawati. Ujenzi wa matundu 5 ya vyoo umekamilika. Utekelezaji umefikia asilimia 95

65,500,000

62,340,140

3,159,860

Timu ya ukaguzi inashauri Kamati ya Ujenzi kuongeza taa za kwenye madarasa yote matatu ziongezwe ili kuwepo na mwanga wa kutosha kwani kwa sasa kila darasa kumewekwa taa 3 zile ndogo.
2.2.3
Ujenzi wa Mabweni 2 ya wanafunzi katika shule ya sekondari Isimila.
Kijiji cha Kaning’ombe
Ujenzi upo katika hatua ya kupandisha kuta na shimo la choo limeshachimbwa. Utekelezaji umefikia asilimia 35.

150,000,000

37,154,385

112,845,615
Ufuatiliaji wa karibu ufanyike kwani kasi ya utekelezaji hairidhishi kulingisha na muda walioanza ujenzi na muda ulibakia hadi kukamilisha ujenzi.

 
2.3 SEKTA YA AFYA




2.3.1
Ujenzi/Upanuzi wa kituo cha afya Idodi  ambao unahusisha majengo matano (Nyumba ya Mtumishi, maabara, wodi ya kina mama, jengo la upasuaji na jengo kuhifadhia maiti)
Kijiji cha Idodi
  • Nyumba ya Mtumishi imeshapauliwa. Kazi zinazoendelea ni upigaji wa plasta nje na ndani.
  • Maabara imeshapauliwa, kuwekewa mbao za dari. Kazi zinazoendelea umaliziaji wa kupiga plasta nje ya jengo.
  • Wodi ya kina mama imeshapauliwa na kuwekewa mbao za dari. Kazi zinazoendelea umaliziaji wa kupiga plasta nje ya jengo.
  • Jengo la upasuaji limeshapauliwa na kuwekewa mbao za dari. Kazi zinazoendelea umaliziaji wa kupiga plasta nje ya jengo.
  • Jengo la kuhifadhia maiti (mortuary) limeshapauliwa na kuwekewa mbao za dari. Kazi zinazoendelea umaliziaji wa kupiga plasta nje ya jengo.
Kazi nyingine zinazoendelea katika majengo yote ni ununuzi wa vifaa kwa ajili ya kuweka dari na vifaa vingine

400,000,000

180,158,780

219,841,220
Kasi ya ujenzi iongezwe ili umaliziaji wa ujenzi ukamilike kwa muda uliopangwa na kuanza kutoa huduma. Aidha Timu ya ukaguzi inashauri Kamati ya ujenzi kazi zinazoweza kufanyika kwa wakati mmoja ni vizuri zikafanyika kwa pamoja, Pia  kuwa na “provisional” ya mfumo wa  malipo wa GOTHOMIS.
 
 
          2.4  SEKTA YA MAJI
 
 
 
 
2.4.1
Ujenzi wa mradi wa maji kwa kufunga solar panel 8, ununuzi wa pump, ujenzi wa pump house & tank tower, ununuzi wa tank la maji lita 5000 na ujenzi wa vituoa vitatu vya kuchotea maji shule ya msingi Mlambalasi
Kijiji cha Kipera
Ujenzi wa mradi huu umekamila na maji yanatoka kwenye vituo vyote vya kuchotea maji. Utekelezaji umefikia asilimia 99.

68,503,000

0

68,503,000


2.4.2
Ujenzi wa mradi wa maji kwa kufunga  ununuzi wa pump, ujenzi wa pump house & tank tower, ununuzi wa tank la maji lita 5000 na ujenzi wa vituo vitatu vya kuchotea maji shule ya msingi Kiponzero
Kijiji cha Kiponzero
Ujenzi wa mradi huu umekamilka na maji yanatoka kwenye vituo vyote vya kuchotea maji. Utekelezaji umefikia asilimia 99
Kuongeza kituo kimoja kwa ajili ya wananchi ili wasiende kuchota maji kwenye vituo vilivyopo kwa ajili ya wanafunzi.
2.4.3
Ujenzi wa vinawia mikono (Hand washing facilities) 10 katika shule za msingi za Chamgogo, Kiponzero, Mlambalasi, Mboliboli, Magombwe, Isele, Luganga, Makuka, Itunundu na Kidamali.
Vijiji vya Chamgogo, Kiponzero, Mlambalasi, Mboliboli, Magombwe, Isele, Luganga, Makuka, Itunundu na Kidamali.
Ujenzi wa vinawia mkono 10 umekamili kwa ailimia 100.
3,000,000

3,000,000

0

Mradi unatumika
2.4.4
Ujenzi wa mradi wa maji Izazi-Mnadani
Kijiji cha Izazi na Mnadani
Kisima kimeshachimbwa, nyumba ya pampu imeshajengwa, ulazaji mabomba na kuyafukia umekamlika, vituo 18 vya kuchotea maji vmekamilika. Pia katika kitongoji cha Ihanyi kisima kimeshachimbwa (sio kwenye kandarasi hii), ujenzi pump house umekamilika. Kazi zilizobaki ni ufungaji wa pump ya umeme ambao unasubiri usambazaji wa umeme katika kijiji cha Izazi, umaliziaji wa tank la lita 100,000, kuweka umeme wa jua katika kisima kilichopo Ihanyi, kuweka tanki la lita 5000 na kufanya umaliziaji katika maneo mengine. Utkelezaji umefikia asilimia 85.
725,056,271.01

535,447,890.76

189,608,380.25

Kufanya   manunuzi   ya   pampu   haraka   kwa   kufuata   taratibu   zote   kwani umeme   umekwishafika   hadi eneo   lililochimbwa visima   ili   mradi huu   uanze kutoa huduma   kwa   wananchi.
2.4.5
Ujenzi wa mradi wa maji Migoli-Mtera
Kijiji cha Migoli na Mtera
Kisima kimeshachimbwa, pump house imeshajengwa, ulazaji mabomba na kuyafukia umekamlika, vituoa 20 vya kuchotea maji umekamilika na kufukia bomba kwa zege kwa maeneo yenye makorongo umefanyika. Pia katika soko la Migoli kisima kimechimbwa, ujenzi wa nyumba ya pampu umekamilika, pump ya umeme imefungwa, tanki la lita 5000 limewekwa na maji yanatoka. Aidha, kwa upande wa Mwanyengo umefanyika ujenzi wa pump house, uwekaji wa ‘solar pannel’ 8, kufunga pump controller na kufanya maboresho mengine. Kazi zilizobaki ni ufungaji wa pump ya umeme ambao unasubiri usambazaji wa umeme katika kijiji cha Izazi na kufanya umaliziaji katika maneo mengine. Utekelezaji umefikia asilimia 90.
1,385,930,662.02

979,091,560.92

410,839,101.10

Katika ukaguzi huo timu ilibaini kuwepo kwa makorongo mengine ambayo awali survey ilipofanyi kahayakuwepo. Hivyo timu ya ukaguzi inashauri Mhandisi wa Maji (W) katika eneo hilo   mabomba yafukiwe kwa kumiminwa zege katika makorongo yaliyojitokeza.

 

Jumla Kuu

 
3,237,405,933.03
 
2,099,554,356.68
 
1,141,851,576.35
 

Naomba kuwasilisha.

Robert M. Masunya

Mkurugenzi Mtendaji (W)

Iringa

 

Matangazo

  • Matokeo ya Kidato cha pili na Kidato cha nne 2020 haya hapa January 15, 2021
  • TANGAZO UPANGISHWAJI WA MAJENGO YA HALMASHAURI YA WILAYA YA IRINGA. December 14, 2020
  • UZINDUZI WA BARAZA LA MADIWANI 2020/2025 December 14, 2020
  • Tangazo la ujio wa Madaktari bingwa kutoka Ujerumani katika Kituo cha Afya cha Ifunda Mission. February 06, 2020
  • Tazama zote

Habari Mpya

  • Muwezezaji wa Mrati wa World Vision Wasa Bi.Gaudencia Mushi akiwa katika picha ya pamoja na wazazi na watoto waliopatiwa vitimwendo katika kata ya Wasa

    November 26, 2020
  • Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mh.Richard Kasesela pichani akifungwa skafu na skauti alipowasili katika shule ya Sekondari Ilambilole

    November 04, 2020
  • Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mh.Richard Kasesela pichani akifungwa skafu na skauti alipowasili katika shule ya Sekondari Ilambilole

    November 04, 2020
  • Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mh.Richard Kasesela akiwa katika picha ya pamoja mara baada ya kuzindua baraza la watoto la Halmashauri ya Wilaya

    October 20, 2020
  • Tazama zote

Video

Katibu Mkuu Wizara ya Kilimo Bw.Gerald Kusaya azindua rasmi ghala la Isele
video

Viungo vya haraka

  • Dashibodi ya Mapato
  • Salary slip

Viungo vinavyohusiana

  • Ofisi ya Rais-TAMISEMI
  • Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi Stadi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Ofisi ya Rais-Wakala ya Serikali Mtandao
  • Ofisi ya Rais -Utumishi na Utawala Bora
  • Sekretariati ya ajira
  • Ofisi ya Takwimu ya Taifa
  • Tovuti kuu ya takwimu huria
  • Tovuti Rasmi ya Rais

Idadi ya watembeleaji duniani

world map hits counter

Idadi ya Watembeleaji

https://bachelorthesiswritingservice.com

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Mtaa wa Gangilonga

    Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa

    Simu ya mezani: 026-2702828/2702585

    Simu ya mkononi: 0767778106

    Barua pepe: ded@iringadc.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • MMM
    • Ramani ya tovuti
    • Huduma

Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa