Kamati ya Fedha, Utawala Na Mipango ya Halmashauri ya Wilaya ya Iringa imefanya ziara ya kutembelea miradi mbalimbali inayotekelezwa ikiwemo ujeshi wa shule mpya ya sekondari katika kijiji cha Ugwachanya na kufurahishwa na kazi inayoendelea hapo. Ziara imefanyika Oktoba 31, 2024.
Akizungumza wakati wa ziara hiyo Mwenyekiti wa kamati Mhe. Kindole ameridhishwa na kazi inayoendelea na kuongeza kuwa kama ilivyoanza vema na tumepongeza, vivyo hivyo umaliziaji unapaswa kuwa mzuri ili uakisi kinachoonekana kwa sasa.
Shule mpya ya sekondari Ugwachanya imepokea kiasi cha Tsh. 583,180,028/- kutoka Serikali kuu ambazo zimelenga kukamilisha kazi zifuatazo;
Shule hii inatarajiwa kukamilika na kupokea wanafunzi wa kidato cha kwanza kuanzia Januari 2025, ambapo awali wanafunzi walilazimika kutembea umbali mrefu hadi shule ya sekondari iliyopo kijiji cha Tanangozi.
Maeneo mengine yaliyotembelewa na kamati hii ni Karakana ya Halmashauri, Kituo cha ukusanyaji wa mapato Wenda na Zahanati ya kijiji cha Mfukulembe.
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa