Mhe. Kheri Aongoza Mkutano wa Jumuiya Hifadhi ya Wanyamapori (MBOMIPA)
Mkuu wa Wilaya ya Iringa Mheshimiwa Kheri James ameongoza Mkutano Mkuu wa Baraza la Wajumbe wa Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori (MBOMIP), na Wadau wake wa uhifadhi kwa lengo la kujadili na kupeana maelekezo ya yatakayosaidia kuendeleza na kustawisha Hifadhi za Wanayampori kuchochea maendeleo kwa maslahi ya Wananchi na Taifa kwa ujumla.
Akizunguzmza katika mkutano huo uliofanyika Oktoba 23, 2023 katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo Kikuu Huria Manispaa ya Iringa Mhe. Kheri amewataka viongozi wa Jumuiya ya MBOMIPA kuhakikisha kwamba, fedha wanazozitoa kusaidia jamii zilizo karibu na Hifadhi hizo, zielekezwe kwenye huduma na maeneo ambayo yanagusa watu wengi ikiwemo Elimu, Afya, na huduma nyingine muhimu kwa jamii.
Sambamba na hilo, Mhe. Kheri amewataka Viongozi, Wajumbe wa Jumuiya ya Hifadhi ya Wanyamapori kushirikiana na Wadau wengine kupambana dhidi ya ujangiri, kutokomeza uharibufu wa Hifadhi ambao unapelekea kupoteza maliasili ya wanyamapor,i ambao ndio hitaji kubwa linapokuja suala la Utalii katika Mkoa wa Iringa Taifa kwa ujumla.
“Kwenye hili Seirkali ipo, pale mnapoona juhudi zenu haziwezi kufanya vizuri zaidi msiogope kuomba msukumo wa Serikali na vyombo vyake, ili kufanikisha malengo ya kupambana na ujangiri kwenye maeneo yetu”
“Tukiuchekea ujagiri katika maeneo haya, muda siyo mrefu Hifadhi hizi zitakuwa majanga yasiyokuwa na chochote, kwa hiyo lazima tusimame kidete kutokomeza ujangiri na uharibifu kwenye Hifadhi zetu za Wanayamapori”. Amesema Mhe. Kheri
Kijiji cha Ihemi
Anuani ya posta: Po.Box108 Iringa
Simu ya mezani: 026-2702828/2702585
Simu ya mkononi: 0757 364 994
Barua pepe: ded@iringadc.go.tz
Haki miliki @ Halmashauri ya Wilaya ya Iringa. Haki zote zimehifadhiwa